Tuzo yampa mzuka straika Guinea

Muktasari:

Guinea ilipoteza mchezo huo kwa mabao 2-0 yaliyoifanya Cameroon iongoze kundi B la mashindano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) yanayoendelea nchini.

Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya kutangazwa mchezaji bora wa mechi baina ya Cameroon na Guinea, mshambuliaji Algassime Bah ametamba kuwa itampa molali ya kuibeba timu yake kwenye mechi zijazo.

Guinea ilipoteza mchezo huo kwa mabao 2-0 yaliyoifanya Cameroon iongoze kundi B la mashindano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) yanayoendelea nchini.

Bah alisema kuwa anaamini kuwa kupata tuzo hiyo kutampa chachu ya kufanya vizuri zaidi ili timu yake iweze kupata mafanikio kwenye mechi zijazo.

"Nafurahi kupata tuzo hii ambayo ni kitu kikubwa kwangu. Ndoto zangu ni kujituma zaidi kwenye mechi zijazo na nitafurahi zaidi kama nitapata tuzo kama hii lakini kikubwa ni kuisaidia timu yangu," alisema Bah.