Tshishimbi nahodha mpya Yanga

Muktasari:

Tshishimbi sasa anaziba nafasi ya mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye alikuwa nahodha wa timu hiyo kabla ya kutimkia Simba.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefanya maamuzi kamili akimteua kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kuwa nahodha mpya wa timu hiyo.
Tshishimbi anachukua nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib ambaye amerejea klabu yake ya zamani ya Simba .
Zahera amesema tayari amefanya maamuzi ya kumpa cheo Tshishimbi kuwa nahodha mpya wa Yanga.
Zahera amesema maamuzi hayo yamekubalika kwa wachezaji wote ambao wamekubaliana na uteuzi huo.
Kocha huyo Mkongomani amesema kiungo huyo amekuwa na sifa za kutosha kupewa majukumu hayo.
Aidha Zahera amesema msaidizi wa Tshishimbi atabaki kuwa beki wa kulia Juma Abdul ambaye hata hivyo hajajiunga na timu hiyo.
Zahera amesema Abdul na beki mwenzake Andrew Vincent 'Dante' watamaliza changamoto zao kisha wataungana na timu hiyo.
Amesema amezungumza na wachezaji hao na kuelewa changamoto zao na zitamalizwa haraka.