Tshabalala: Mtibwa Sugar wazuri ila Simba ushindi upo

Thursday September 12 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Beki na nahodha wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amekiri wapinzani wao Mtibwa Sugar wanawapa wakati mgumu ila wamejiandaa kushinda kushinda mechi hiyo.

Tshabalala alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwako, lakini wana kila sababu ya kuibuka na ushindi.

"Mechi ngumu, Mtibwa ni wazuri na huwa wanatusumbua katika mechi zetu sasa ni jukumu letu kufanya kweli, kuondoa dhana hiyo," alisema Tshabalala.

Alisema, wachezaji wote wana ari na morali ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

Huo ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara kwa Simba baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Advertisement

Advertisement