TryAgain-Tumetimiza wajibu

Muktasari:

  • Kaimu Rais huyo wa zamani wa Simba alisema kinachofuata kwa sasa ni wao viongozi kusubiri marejesho ya kocha baada ya kusonga mbele ili kuona kwa namna gani wafanye vizuri.

MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema ahadi walizozitoa kwa wachezaji wao pamoja na maandalizi kambambe vimechangia kuibeba timu hiyo kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba iliweka rekodi kwa mara nyingine tena kutinga robo fainali baada ya kuilaza AS Vita ya DR Congo mabao 2-1, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Viongozi tulishikamana. Awali tulikuwa na malengo ya kufika makundi lakini tulivyoona tuna timu nzuri tulikaa chini na kuweka mikakati ya namna ya kuvuka hatua hiyo.

“Hakuna kingine zaidi ya maandalizi mazuri pamoja na ahadi kwa wachezaji wetu, vyote hivyo vimeifanya leo hii Simba inaipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa,” alisema Try Again.

Kaimu Rais huyo wa zamani wa Simba alisema kinachofuata kwa sasa ni wao viongozi kusubiri marejesho ya kocha baada ya kusonga mbele ili kuona kwa namna gani wafanye vizuri.