Trans Camp walia na waamuzi

Thursday November 7 2019

By Mwandishi wetu

KOCHA wa Trans Camp, Steven Matata amesema watahakikisha mchezo wao wa keshokutwa Jumamosi dhidi ya Gwambina FC ugenini wanashinda ili kujichomoa mkiani kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hukua akisema waamuzi hawatendi haki kwa kupendelea baadhi ya timu.

Trans Camp ina pointi tatu inashika mkia kwenye Kundi B huku ikiwa ndio timu pekee ambayo haijashinda mchezo wowote kwenye kundi hilo.

Matata amesema waamuzi wengi wanaochezesha ligi hiyo wanatia hasira na wakati mwingine kusababisha hata makocha kutaka kuchukua maamuzi magumu hivyo kulitaka Shirikisho la

Soka Tanzania (TFF) kuitupia macho ligi hiyo kwani waamuzi wengi wana njaa.

“Kweli hatujisikii vizuri kuona tunashika mkia lakini ndio timu pekee ambayo hatujashinda. Hatukati tamaa kwani kwa sasa tuko ugenini na mchezo uliopita tulitoka sare baada ya

pamba FC kusawazisha dakika za mwisho.

Advertisement

“Tunaendelea kupambana ili kujinasua mkiani, naamini kama tutaifunga Gwambina kwao tutafikisha pointi sita hivyo tutapunguza pengo la pointi na walio juu yetu na pia tutarejesha

morali ya wachezaji wangu kikosini kwani kwa sasa ni kama wamethirika kisaikolojia kutokana na matokeo tunayopata”alisema Matata.

Aliongeza” Yaani tatizo kubwa kwenye hii hii ni waamuzi, wengi wana njaa na wanachezesha wanavyotaka hadi wakati mwingine unaweza ukapata hasira na kutaka kufanya kitu

ambacho kinaweza kukushushia heshima kama kocha kwa sababu ya hao waamuzi.

“Hii yote inatokana na kwamba FDL haionyeshwi kwenye televisioni kama Ligi Kuu ambapo waamuzi wengi wanaogopa kwani Azam Tv inamulika madudu yote wanayofanya

uwanjani na mwisho wa siku wanafungiwa , huku kwetu hakuna ufuatiliaji ndio maana wanachezesha wanavyotaka na kuziumiza baadhi ya timu”alisema Matata.

Advertisement