Tottenham wapambana na Arsenal kwa Saliba

Muktasari:

Spurs pia inatajwa kumuwekea mezani beki huyo bonasi kibao ili kumshawishi asaini upande wao aachane na Arsenal ambao wanasuasua kutoa mkwanja, japokuwa nyota huyo anatajwa zaidi kuwataka Washika bunduki hao.

VIGOGO vya soka England, Tottenham Hotspur na Arsenal wameingia vitani kuwania saini ya kinda, William Saliba anayekipiga katika klabu ya Saint-Etienne nchini Ufaransa.

Kinda huyo anayetajwa kuwa beki kitasa, anawaniwa na Spurs ambao wameweka mezani kitita cha Pauni 26.9 mezani wakitaka saini yake, huku Arsenal wakimhitaji kwa mkopo.

Hata hivyo, Tottenham wanatajwa kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kumyakua mchezaji huyo ambaye wakati wowote atamwaga wino katika kikosi chao, licha ya kwamba kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na Arsenal.

Spurs pia inatajwa kumuwekea mezani beki huyo bonasi kibao ili kumshawishi asaini upande wao aachane na Arsenal ambao wanasuasua kutoa mkwanja, japokuwa nyota huyo anatajwa zaidi kuwataka Washika bunduki hao.

Saliba ambaye ameitumia Saint-Etienne mara 16 msimu uliopita katika Ligi Kuu Ufaransa, anakwenda Spurs kuziba pengo la Toby Alderweireld, anayetajwa kutaka kutimkia Manchester United au Roma, ambapo Spurs inataka kuachana naye kwa kuwa amegomea mkataba.