Top six EPL njiapanda

Muktasari:

Maurizio Sarri hajui nini kitafuata kwenye mechi ijayo kama ataendelea kuwapo Stamford Bridge au atatupiwa mabegi yake na kusaka maisha sehemu nyingine. Ligi Kuu England ina mambo yasiyoeleweka tu kwa sasa. Eden Hazard haeleweki kama ataendelea kubaki The Blues baada ya msimu kumalizika. Hilo linamkabili pia Mohamed Salah huko Anfield.

LONDON, ENGLAND.LIGI Kuu England hakueleweki. Mambo mengi yapo njiapanda.

Unajua kwanini? Pep Guardiola na Jurgen Klopp hawaelewi kwenye vita yao ya ubingwa. Mambo ni mengi kwelikweli.

Kingine kisichoeleweka ni kuhusu Top Four. Man United, Arsenal na Chelsea wote wanabambania ‘Top Four’.

Mambo hayaeleweki. Kocha Ole Gunnar Soskjaer haelewi hatima yake huko Old Trafford kama atapewa kibarua cha moja kwa moja mwisho wa msimu, au atafunguliwa mlango wa kurudi kwao Norway.

Maurizio Sarri hajui nini kitafuata kwenye mechi ijayo kama ataendelea kuwapo Stamford Bridge au atatupiwa mabegi yake na kusaka maisha sehemu nyingine. Ligi Kuu England ina mambo yasiyoeleweka tu kwa sasa. Eden Hazard haeleweki kama ataendelea kubaki The Blues baada ya msimu kumalizika. Hilo linamkabili pia Mohamed Salah huko Anfield.

Kama Liverpool itakuwa bingwa msimu huu na kisha vigogo wengine wa Ulaya kama Barcelona na Real Madrid zikaleta ofa ya kumtaka Mo Salah, haieleweki kama staa huyo atakubali kuendelea kubaki kwenye kikosi ha Reds. Hii ndio njiapanda ya Ligi Kuu England msimu huu.

Mauricio Pochettino jina lake linatajwa huko Man United na Real Madrid. Mashabiki wa Tottenham Hotspur ipo njiapanda juu ya kocha wao kama atabaki kwenye kikosi chao au atafungasha virago vyake na kuondoka, huku ikiwa haeleweki kama atatimkia Old Trafford au ataenda zake Santiago Bernabeu.

Mashabiki wa Spurs inavurugwa zaidi kuhusu hatima ya mastaa wao Harry Kane, Dele Alli na Christian Eriksen kama wataendelea kubaki kwenye timu Pochettino akiondoka. Hivi ndivyo timu za Big Six zilivyojaa mambo mengi yenye utata.

Vipi kama Liverpool itamwamini tena Klopp na kutumia pesa nyingi kama itashindwa kubeba taji msimu huu. Haijulikani kitu gani kitamfanya Hazard aondokane na mawazo ya kwenda Real Madrid. Mashabiki wanavurugwa. Hawafahamu baada ya msimu huu nini kitatokea kwenye Big Six.

Guardiola hana uhakika wa kuhusu straika wake namba moja, Sergio Aguero kama ataendelea kubaki kwenye timu hiyo endapo watashinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Akiondoka, nani atakuja kuchukua mikoba yake kwenye kufunga hasa ikizingatiwa kwamba Gabriel Jesus ameshindwa. Ndio hivyo, Ligi Kuu England msimu huu ni pasua kichwa!