Tizi la Mkwasa Yanga usipime

Muktasari:

Baada ya zaidi ya miezi miwili ya Ligi Kuu Bara pamoja na michezo mingine kusimama kutokana na ugonjwa wa covid 19, timu mbalimbali zimeanza mazoezi.

Kikosi cha wachezaji wa Yanga, kimeanza kujifua jioni ya leo katika uwanja wa Shule ya Sheria Ubungo jijini nyuma ya kituo cha Daladala cha Mawasiliano (Simu 2000).

Mazoezi hayo yalianza saa 10:30 jioni chini ya kocha msaidizi, Boniface Mkwasa.

Mara baada ya kufika uwanjani wachezaji walibadilisha nguo na kuingia katika eneo la kuchezea ambapo walizungumza kwa muda mfupi na kuanza mazoezi.

Wachezaji wa Yanga, walianza mazoezi mepesi ya kunyoosha viungo, kukimbia kwa mwendo wa kawaida wakiwekwa katika makundi manne zoezi ambalo walilifanya kwa dakika takribani 10.

Baada ya kumaliza zoezi hilo waliwekwa katika makundi manne tena ambayo walitakiwa kukimbia kwa spidi.

Walifanya zoezi hilo kwa dakika kumi, na baada ya hapo wakipumzika kwa wachezaji kwenda kunywa maji ili kuendelea na mazoezi mengine.