Timu za Bunge Tanzania zaanza kwa Kishindo

Muktasari:

Hii ni michezo ya tisa ya Mabunge ya Afrika Mashariki, ambapo washiriki ni Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na pia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani EALA (East Africa Legislative Assembly).

Dar es Salaam. Timu za Bunge Sports Club za soka, mpira wa  wavu ( wanawake ) na netball zimekuwa gumzo katika jiji la Bujumbura baada ya kushinda michezo yote mitatu leo Disemba 6.

Katika michuano hiyo inayoendelea Bujumbura nchini Burundi katika mchezo wa soka na kuwaduwaza EALA kwa kuwafunga mabao 2-0, mpira wavu (wanawake) waliwafunga EALA seti 3-0, wakati netball Bunge Queens iliwafunga Kenya magoli 52-29.
Katika michezo hiyo ya tisa ya Mabunge ya Afrika Mashariki, walikuwa ni Bunge Queens walioanza kwa ushindi baada ya kuwapoteza kabisa Kenya kwa kuwalaza magoli 52-29 kwenye mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Taifa cha Ualimu.
Timu ya mpira wa wavu (wanawake) ikafuata nyayo kwa kuwagaragaza EALA seti 3-0.
Katika soka Bunge la Tanzania (Ndugai Boyz) wakawafunga Bangalore EALA kwa mabao 2-0, katika mchezo ambao mashabiki walibaki wakijiuliza ilikuwaje baada ya kuona bingwa mtetezi Bunge la Uganda likipoteza mchezo huo.
Kwa mwaka huu timu shiriki ni wenyeji Burundi, Uganda, Tanzania, Kenya na EALA,  nchi zilizokosekana ni Rwanda na Sudan Kusini.
Michezo inayoshindaniwa ni soka, Netball, mpira wa wavu, riadha na Kuvuta Kamba, michezo imefunguliwa Jumamosi 1 Desemba na inatarajia kumaliza 9 Disemba.
Timu za Bunge Sports Club zimeendelea kutamba katika mji wa Bujumbura, nchini Burundi katika mchezo wa soka na kuwaduwaza EALA kwa kuwafunga mabao 2-0, mpira wavu (wanawake) waliwafunga EALA seti 3-0, wakati netball Bunge Queens iliwafunga Kenya magoli 52-29.