Tiboroha akomaa na jezi Yanga

Muktasari:

Uchaguzi mdogo wa Yanga SC wa kuziba nafasi za mwenyekiti,  makamu na wajumbe, unatarajiwa kufanyika Jumapili ya Januari 13.

Dar es Salaam. Wakati mgombea nafasi ya Mwenyekiti Yanga,
Mbaraka Igangula akidai kudhibiti matumizi ya fedha za za klabu hiyo, mpinzani wake Dk Jonas Tiboroha amesema atahakikisha timu hiyo inanufaika na mauzo ya jezi zake.
Tiboroha amesema biashara ya jezi ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya fedha kwa klabu nyingi zilizoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika.
Katibu huyo wa zamani wa Yanga, alisema kama akipewa ridhaa ya kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo atadhibiti mianya yote ya wizi unaofanyika katika upande huo.
"Ifike wakati watu watambue thamani ya jezi zenye nembo ya
Yanga, nitalitolea macho hili suala hakutakuwa na muuza jezi
ambaye hana mahusiano na Yanga," alisema Tiboroha na kuongeza.

"Mauzo ya jezi ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato ambavyo vinaweza kuisaidia klabu yetu kujiingizia kipato."