Tiboroha aendelea kuunguruma Yanga

Muktasari:

  • Uchaguzi mdogo wa Yanga SC wa kuziba nafasi za uenyekiti,  makamu na wajumbe,  unatarajiwa kufanyika Jumapili ya Januari 13.

Dar es Salaam. Ikiwa leo Alhamisi ni siku ya pili ya kampeni za Dk Jonas Tiboroha amesema tatizo kubwa la Yanga SC si fedha ni kupungukiwa viongozi.

Tiboroha anayeomba ridhaa ya kuwa mwenyekiti,  alisema Yanga imebakiwa na viongozi wanne pekee kati ya 12 hivyo ni ngumu kwa uchache wao kuingoza klabu hiyo.

 "Mzigo kwao ni mkubwa na wanahitaji msaada hata hivyo niwapongeze kwa kuendelea kusalia kwenye klabu maana wapo ambao waliamua kuondoka kwa kuachia ngazi, " alisema Tiboroha.

Mmoja wa wajumbe ambao wapo upande Toboroha, Chris Kashililika anayetokea Mkoa wa Songwe,  amesema ni vyema wamacha wa Yanga kutofanya makosa siku ya Jumapili.

"Tunaweza kuivusha Yanga kikubwa ni wanachama kutuamini kupitia vipaumbele vyetu sita ambavyo tutavitekeleza kwa kipindi kifupi," alisema.

Vipaumbele sita  vya kambi ya Tiboroha vimejikita kwenye mabadiliko ya kimfumo kama jambo la kwanza ambalo litaambana na kurudisha klabu kwa wanachana, kujenga na kuimarisha taasisi.

Mengine uwekezaji na biashara, kuimarisha matawi, kuimarisha mifumo ya uendeshaji wa timu na ushirikiano na washirika.