Team Mafisi wamtesa Shetta

Friday November 23 2018

 

By Rhobi Chacha

MSANII wa muziki Bongo, Shetta amesema kuwa ataendelea kumpa binti yake Qayllah, malezi bora ikiwemo kumweka mbali na wanaume ili wasimrubuni.

Shetta ambaye kwa sasa ametamba na ngoma yake ya ‘Namjua’ ameliambia Mwanaspoti kuwa, binti yake huyo atakapokuwa mkubwa kamwe hatakuwa tayari kuona akidanganywa na wanaume kwa kuwa, wengi wapo kwa ajili ya kuharibu maisha ya wanawake.

“Nasimama hapa kama mzazi na sio msanii, kiukweli ninavyoona muonekano wa baadhi ya wanawake kwa sasa asilimia kubwa wanaharibiwa maisha na kitabia na wanaume, hivyo nitakuwa makini sana na mwanangu. Baba yake nina kila kitu kwa ajili ya kumfanya aishi vizuri hivyo, asidanganyike na wanaume akaingia kwenye mitego,” alisema

Aidha, Shetta amesema moja ya vitu alivyokuwa akitamani katika maisha yake ni kujaliwa mtoto akiwa katika umri mdogo na amzingatie katika maadili mema yanayostahili katika jamii.

Advertisement