Tazama Pepe Reina alipocheza kiungo

Muktasari:

Liverpool wakicheza mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Kaiserslautern huko Liechtenstein kuelekea msimu wa 2006-07, mechi hiyo inonekana kama nafasi ya kina Jermaine Pennant kupata nafasi ya kucheza kwa sababu ndio kwanza alikuwa amejiunga na Liverpool kwa ada ya Pauni 6.7 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND.KIPA wa Manchester City, Ederson amesema matamanio yake ya kuacha nafasi yake ya kukaa golini na kwenda kucheza kwenye sehemu ya kiungo sambamba na wakali kama kina Fernandinho na David Silva – lakini hilo analoliwaza kipa huyo wa Brazil, limeshawahi kufanywa na kipa Pepe Reina wakati huo alipokuwa akiidakia Liverpool.

Ederson alisema hilo katikati ya msimu wa 2018-19, baada ya kwenye mechi moja ya Man City na Wolves, kipa huyu kupanda hadi katikati ya uwanja na kugongeana pasi na wachezaji wake jambo lililomfanya Kocha Pep Guardiola kuwa kwenye presha kubwa kwa uamuzi huo wa kipa wake.

Lakini, kwenye hilo Ederson hakuwa kipa wa kwanza kutoka golini na kwenda na mpira hadi katikati ya uwanja.

Fabian Barthez alifanya hivyo kwenye mechi ya kirafiki akiwa Manchester United, wakati David James alifanya vyema zaidi mwaka 2005 wakati kocha Stuart Pearce alipomtoa golini kwenda kuongeza mashambulizi ya Manchester City kwenye mechi dhidi ya Middlesbrough walipokuwa wakitafuta bao ambalo lingewafanya wafuzu kucheza Kombe la Uefa. Wakati kipa David James anapandishwa mbele kucheza nafasi ya mshambuliaji, kwenye benchi la Man City kulikuwa na straika halisi, Jon Macken.

Mwaka mmoja baada ya tukio hilo la David James, kipa mwingine za wamani wa Liverpool, Reina alipata nafasi ya kucheza ndani na si golini.

Liverpool wakicheza mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Kaiserslautern huko Liechtenstein kuelekea msimu wa 2006-07, mechi hiyo inonekana kama nafasi ya kina Jermaine Pennant kupata nafasi ya kucheza kwa sababu ndio kwanza alikuwa amejiunga na Liverpool kwa ada ya Pauni 6.7 milioni. Wachezaji wengine wa ndani waliokuwa wamejiunga na Liverpool kwa wakati huo walikuwa Craig Bellamy, Fabio Aurelio na Gabriel Paletta. Mechi hiyo ilikuwa na matukio ya kuvutia.

Baada ya kushindwa kufungana kwenye kipindi cha kwanza, timu hiyo ya Ujerumani ilifunga bao kwenye dakika 56, lakini Liverpool wakasawazisha na kufunga la kuongoza kupitia kwa Craig Bellamy na Luis Garcia. Kaiserslautern wakafunga tena na kusawazisha muda mfupi baadaye. Kocha Rafa Benitez alibaki anakuna kichwa baada ya Garcia na Aurelio kuumia na wakati huo tayari walikuwa wamemaliza sub zao zote. Robbie Fowler aliruhusiwa kuingia tena uwanjani, kwa sababu tayari alikuwa ameshatoka, lakini Benitez aliamua kumwingiza kipa Reina katika nnafasi ya kiungo Garcia. Kilikuwa kitu cha kushangaza, lakini mabadiliko hayo nusura yalete matunda mazuri kwa Liverpool.

Reina aliingia akiwa amevaa jezi namba 14, iliyokuwa ikivaliwa na Mhispaniola mwenzake, Xabi Alonso. Muda mfupi tu ndani ya uwanja, Reina alikaribia kufunga mara mbili, baada ya shuti lake la kwanza kupita pembeni kidogo ya goli, kabla ya lile la pili, kupita juu ya goli la wapinzani kufuatia pasi ya Bellamy. Alipokosa bao la pili, mpira ukipita sentimeta chache sana juu ya goli la wapinzani, benchi lote la ufundi la Liverpool lilinyanyuka na kuona vitu matata vinavyofanywa na kipa wao Reina kwa siku hiyo alipocheza kwenye sehemu ya kiungo.

Kaiserslautern wakaja kufunga bao la tatu na kushinda mechi 3-2, lakini kubwa kwa siku hiyo kwenye mchezo huo, ilikuwa Pepe Reina kuonyesha ubora mkubwa akicheza kwenye sehemu ya kiungo na si pale kwenye ile milingoti mitatu ambayo wengi wamezoea kumwona.

Baada ya mechi, mwenyewe alisema: “Nilipata nafasi moja nzuri sana ya kufunga, lakini nikashinda, sasa nafahamu kumbe kufunga si kitu rahisi. Kucheza kwenye kiungo lilikuwa suluhisho pekee kwa sababu tulikuwa tumemaliza sub zetu zote. Ni kawaida kwa mambo kama hayo kutokea, hivyo ilinipasa kufa nya.”

Hiv yo ndi vyo ilivy ok uwa kwa Re ina, je Mhispaniola mwenzake Pep Guardiola ataweza kumpatia nafasi Ederson ya kutimiza ndoto zake za kucheza kwenye kiungo na kutoka golini? Tusubiri.