Tanzanite wakata tamaa mapema

Muktasari:

  • Kocha wa Tanzanite alisema; “Malengo ya ubingwa yameondoka tayari baada ya mechi ya jana (juzi) dhidi ya Panama nilitegemea wachezaji wangu wangefanya jambo la tofauti kwa vile tulikuwa nyumbani, lakini tukafungwa.”

ARUSHA.VIPIGO mfululizo inavyopata katika Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake, vimeikatisha tamaa Tanzanite SC ya jijini hapa, ikiamini imepotezea dira na kiu iliyokuwa nayo ya kubebea ubingwa msimu huu wa kwanza katika ligi hiyo.

Tanzanite ilipokea kipigo chake cha tano kutoka kwa Panama FC ya Iringa na kuzidi kuiacha pabaya timu hiyo iliyopanda ligi hiyo msimu huu sambamba na Yanga Princess ambayo juzi Jumapili ilipigwa ‘wiki’ na watani zao wa Jadi Simba Queens.

Timu hiyo ilichapwa 2-1 na Simba, kisha kulala 6-0 dhidi ya vinara wa ligi hiyo na kubamizwa 2-1 na Yanga kabla ya Mlandizi Queens kuwapigisha kwata 3-0 na juzi tena kupoteza mara ya pili nyumbani 1-0 mbele ya Panama.

Kocha wa Tanzanite alisema; “Malengo ya ubingwa yameondoka tayari baada ya mechi ya jana (juzi) dhidi ya Panama nilitegemea wachezaji wangu wangefanya jambo la tofauti kwa vile tulikuwa nyumbani, lakini tukafungwa.”

Kocha Juma alisema kufungwa kwa mechi zote ni kuzidiwa ujanja na maarifa katika ligi hiyo ambayo wao ni wageni, lakini watapambana ili kutoka eneo la chini wakiwa nafasi ya pili toka