Tanzanite Queens hofu tupu kukabiliana na JKT

Muktasari:

  • Kocha wa Tanzanite Queens, Abdallah Juma alisema uhakika wa kushinda mchezo huo ni mdogo kutokana na kikosi chake kupungua nguvu wakati wa usajili wa dirisha dogo baada ya kuachana na wachezaji wanne huku waliowasajili wakishindwa kuripoti hadi leo kambini.

ARUSHA.TIMU ya soka ya Tanzanite Queens leo Alhamis inawakaribisha vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, JKT Queens mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku wakionekana kukata tamaa ya kupata ushindi nyumbani.

Vipigo hivyo vya mfululizo vimewatia hofu Tanzanite Queens ambao wameapa kupambana kufa na kupona ingawa matumaini yao ya ushindi ni madogo.

Kocha wa Tanzanite Queens, Abdallah Juma alisema uhakika wa kushinda mchezo huo ni mdogo kutokana na kikosi chake kupungua nguvu wakati wa usajili wa dirisha dogo baada ya kuachana na wachezaji wanne huku waliowasajili wakishindwa kuripoti hadi leo kambini.

“Siwezi kusema chochote juu ya matokeo ya mchezo huo maana hatuna nguvu sana katika kikosi chetu kwani kuna wachezaji waliondoka wakati wa dirisha dogo na waliosajiliwa hajaja baada ya kukosa uthibitisho wa leseni kutoka TFF hivyo tuko kwenye wakati mgumu hivyo hatuwezi kusema moja kwa moja kuwa tutashinda mehci hiyo,” alisema kocha huyo.

“Kikubwa mashabiki waje kwa wingi uwanjani kushuhudia burudani ya soka la wanawake, kuna matokea ya aina tatu kushinda, sare na kupoteza hivyo lolote linaweza kutokea,” alisema.