Tanasha wa Diamond: Sihofii kuachwa kama Zari au Hamisa Mobetto

Muktasari:

Tanasha na Diamond wanataraji kupata mtoto hivi karibuni na kumekuwa na kauli nyingi kuwa mrembo huyo atafuata nyayo za watangulizi wake Zari na Mobetto

Mpenzi wa mwanamuziki DiamondTanasha Donna ameweka wazi kwamba haofii kuachwa na mchumba wake huyo.

Tanasha Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliingia ‘live’ na kusema anaona watu wakiandika katika mitandao ya kijamii kuwa anaweza kuchwa na Diamond wakati wowote pindi atakapojifungua kama walivyoachwa wanawake aliowazalisha Zarinah Hassan ‘Zari’ na Hamisa Mobetto hivyo yeye haoifii tukio hilo.

Aidha Tanasha aliendelea kusema, watu wengi wanahangaika kumpa taarifa za matukio mabaya ya nyuma kuhusu Diamond kwani yeye hawezi kumuhukumu mpenzi wake huyo kwa taarifa zilizopita, kwani hata yeye ana mabaya aliyokuwa akiyafanya kabla ya kuwa na Diamond.

“Leo na weka wazi hapa kuhusu mpenzi wangu Diamond, kwanza watu wasihangaike sana kunitag au kunitumia meseji inbox ya Instagram kwa matukio mabaya ya mapenzi yanayomuhusu Diamond, kwani hata mimi nina matukio mbaya vilevile hivyo nimekubaliana nae kwa yote aliyotenda huko nyuma.

“Kuhusu habari za kuniambia kuwa nitaachwa pindi nitakapozalishwa kama walivyofanyiwa wanawake waliopita, kiukweli mimi sihofii kwa hilo tukio hivyo msihangaike sana kulizungumzia hilo suala” alisikika akisema Tanasha.