Tambwe na mkewe ng'aring'ari ndoa ya nguvu

Muktasari:

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amekuwa kwenye kiwango cha juu tangu atue Tanzania akitokea kwao Burundi na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara mara mbili ingawa alipata maulivu msimu uliopita ambayo yalimfanya asing'are msimu huu.

Dar es Salaam. Straika wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe jana Alhamisi alifanikisha zoezi la kumchukua jumla mkewe Raiyan Mohammed baada ya kufunga naye ndoa na kesho Jumamosi kutakuwa na bonge la sherehe maeneo ya Ilala, Boma.
Tambwe ambaye alitua Tanzania na kujiunga na Simba akitokea Vital 'O' ya Burundi kabla ya kutua Yanga anayoichezea mpaka sasa.
Alifanikisha zoezi hilo nyumbani kwa kina Raiyan maeneo ya Buguruni Lozana jijini Dar es Salaam. Sherehe ambazo zilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Yanga kama Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaaya, Mratibu Hafidh Saleh, Meneja Nadir Haroub 'Cannaro' na wachezaji kama, Juma Abdul.
Tambwe na Raiyan wamefanikisha hilo baada ya kukaa kwenye mahusiano na kuishi nyumba moja kwa takribani miaka mitano, sasa wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume anaitwa Ayman ingawa kwa mmchezaji huyo ni wa pili anaye mkubwa aliyemzaa kwao Burundi. 
Itafuata sherehe kabambe itakayofanyika maeneo ya Ilala, Boma jijini Dar es Salaam na baadaye tukio lingine litakuwa nyumbani kwa kina Tambwe nchini Burundi.