Tamasha la dini lampa Tv

Wednesday June 26 2019

 

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam.Tamasha la dini linalojulikana kama "Twenzetu kwa Yesu" limeshudia Bariki Josephat akijishindia zawadi ya Tv kutoka katika kampuni ya Startimes.

Tamsha hilo lilifanyika Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku ikiwa linaanyika kila mwaka kwa lengo la kukutanisha vijana wa kikristo.

Mwaka huu StarTimes walikuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na maelfu ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

StarTimes walitoa zawadi mbalimbali kwa Vijana waliohudhuria tamasha hilo, miongoni mwa zawadi hizo vilikuwemo ving’amuzi vitano vya Antenna vya StarTimes, Smart TV ya StarTimes inch 50 ambayo ilienda kwa kijana Bariki Josephat wa Usharika wa KKKT Mbezi jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia zawadi hiyo Bariki alisema "Nimefurahi kupata zawadi hii, kiukweli nilipokuwa nakuja kwenye tamasha la leo sikutegemea kama kutakuwa na kitu kama hiki, namshukuru sana Mungu pia nawashukuru StarTimes kwa zawadi hii.” .

Zawadi hiyo amekabiziwa leo katika makao makuu ya Startimes Bamaga, Dar es Salaam.

Advertisement

Advertisement