Taifa Stars yawaweka roho juu Watanzania

Muktasari:

Stars walianza kipindi cha kwanza kwa kasi kwa kufika golini kwa Lesotho mara kwa mara na waliweza kutengeneza nafasi dakika ya 18 baada ya kupata mpira ambao ulikwenda kulishwa na Abdallah Kheri ambao ulitoa katika kichwa cha Saimon Msuva ambaye alitoa pasi ikaenda kwa Shabani Chilunda ambaye alipiga tikitaka ambayo ilidakwa.

Timu ya Taifa ya (Taifa Stars) walikuwa ugenini kucheza dhidi ya Lesotho katika Mji wa Maseru katika na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika kilikwenda bila ya miamba hiyo ya Kundi 'L' bila kufungana.
Stars walianza kipindi cha kwanza kwa kasi kwa kufika golini kwa Lesotho mara kwa mara na waliweza kutengeneza nafasi dakika ya 18 baada ya kupata mpira ambao ulikwenda kurushwa na Abdallah Kheri ambao ulitoka katika kichwa cha Saimon Msuva ambaye alitoa pasi ikaenda kwa Shabani Chilunda ambaye alipiga tikitaka ambayo ilidakwa.
Dakika 20 Kheri alifanya makosa kwa kurudisha mpira mfupi ambao alikutana nao straika wa Lesotho aliyemalizia mpira ambao uligongwa mwamba na kuokolewa, dakika 29 Ally Mtoni alipiga faulo ambayo Chilunda aliunganisha kwa kichwa na kwenda nje.
Lesotho walitengeneza nafasi za wazi tatu dakika ya 39 ambayo iliokolewa na Kelvin Yondan, dakika 46 kona ambayo walishindwa kumalizzia na dakika ya 85 makosa ya Aggrey Morris kurudisha mpira mfupi ulionaswa na straika ambaye mpira aliopiga uligingwa mwamba.
Wenyeji Lesotho walipata bao dakika 76 kwa mpira wa kona uliopanguliwa na Manula ambao mabeki walishindwa kuondoa mpira huo.
Stars walionekana kuwa na mapungufu haswa katika safu ya ushambuliaji kwani walitengeneza nafasi ambazo Chilunda pekee yake ndio alionekana kukosa na kuwasumbua safu ya ulinzi ya Lesotho lakini mastraika wengine walionekana kuwa chini ya ulinzi.
Msuva ambaye alicheza kama straika msaidizi nae alikuwa chini ya ulinzi na muda mwingi alionekana kufanya mashambulizi katika eneo ambalo si la hatari, winga wa kushoto alikuwa Gadiel Michael ambaye nae muda mwingi alionekana katika kukaba na si kushambulia.
Himid Mao ambaye alicheza katika winga wa kulia nae muda mwingi alionekana akisaidia kukaba viungo wa kati na katika kushambulia alikuwa akionekana mara kadhaa, katika kiungo mshambuliaji kulikuwa na Mudathir Yahya ambaye nae alionekana kuwa imara katika kukaba na si kushambulia.
Mabadiliko ya kuingia Shiza Kichuya, Faisal Salum na John Bocco hayakuwa na tija pengine kutokana na muda ambao waliingia tofauti na wakati timu ilipokuwa inahitaji nguvu haswa katika eneo la ushambuliaji.
Kocha wa Stars Emmanuel Amunike alionekana kuwa na mpango wa kuzua muda mwingi kwani licha ya kutokuwa na mastraika asilia lakini alianza na mabeki sita wenye asili ya kucheza kati Yondan, Morris, Kheri na Nyoni.
Lakini katika eneo la kushambulia alicheza Mudathir na Mao ambao wote kiasili ni viungo wakabaji, Michael ni beki wa kushoto, kwa maana hiyo washambuliaji walioanza walikuwa wawili Chilunda na Msuva.
Stars walionekana kucheza mipira mirefu katika eneo la ushambuliaji lakini huenda haikuwa njia sahihi ya kushambulia kwani mastraika wao wawili Chilunda na Msuva wote si warefu kulinganisha na mabeki wa Lesotho.