Taifa Stars yawarudisha nyota wa Simba Dar es Salaam

Tuesday July 23 2019

 

By Doris Maliyaga

Rostenburg.  Wachezaji saba wa Simba wanaocheza timu ya Taifa Stars wanatarajia kuondoka Afrika Kusini kesho, Jumatano tayari kujiunga na timu ya Taifa Stars.

Wachezaji wa Simba wanaotakiwa kuripoti kambini Stars kujiandaa na mchezo dhidi ya Kenya ni pamoja Ibrahim Ajibu,  Jonas Mkude, John Bocco,  Gadiel Michael,  Aishi Manula, Hassan Dilunga na Erasto Nyoni.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema wachezaji hao watalitakiwa kuondoka mapema lakini kutokana na aina ya usafiri waliotumia inabidi waondoke Jumatano.

"Tunatarajia watarudi Tanzania siku ya Jumatano kwa ajili kuungana na timu ya Taifa," alisema Magori.

Magori alisema imebidi kuwa hivyo kwa sababu ndege waliyotumia ya ATCL haisafiri kila siku.

Akizungumzia kambi hiyo Magori ambaye aliongozana na shabiki pamoja na mwanachama wa Simba anayejulikana kwa jina la Matthew Shayo na kuangalia mazoezi ya jioni.

Advertisement

Kwa akashusha pumzi kutokana na umbali aliokutana nao hadi kufika mahali ambapo Simba imeweka kambi.

"Nimefurahi kufika hapa kwanza mazingira ya kambi ni tulivu na yamejificha jambo linalofanya wachezaji kuwa katika hali ya utulivu," alisema Magori.

Kuhusu ratiba ya CAF ilivyo wachanganya kwani walitegemea Simba itacheza mzunguko wa pili, lakini wameanza wa kwanza.

"Hatukutegemea kitu kama hicho jambo lililomfanya kocha abadili programu yake haraka na sasa wameanza kucheza.

Aussems ameanza programu ya timu yake kuchezea mpira kitimu, akisisitiza mbinu na ufundi tofauti na ilivyokuwa awali.

 

Advertisement