Taifa Stars itawabeba Wabongo kucheza Ulaya

Monday September 10 2018

 

MZUNGU wa African Lyon, Victor Da Costa amesema kitakachotoa zaidi nafasi kwa wachezaji wa Kitanzania kucheza soka la kulipwa barani Ulaya ni kufanya vizuri kwa Timu ya Taifa, Taifa Stars.

Costa ambaye amekuwa akitumika kwenye kikosi cha African Lyon kama mshambuliaji anayesaidiana na Haruna Moshi Boban anaamini Tanzania ni nchi yenye vipaji vingi vya soka.

“Inawezekana mawakala wengi wa soka wanaibeza Tanzania kwa sababu ipo chini kwenye viwango vya ubora wa soka duniani. Kama ingekuwa kuanzia nafasi ya 80 kupanda juu, ingesaidia.

“Vinginevyo itaendelea kutumia nguvu kubwa, muda mfupi ambao nimekuwa hapa nimegundua hii nchi ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza hata kwenge ligi ya nyumbani, France Ligue 1,” alisema Costa.

Costa ambaye anafanana kimwonekano na mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud ni mzaliwa wa Ureno, aliyekulia na kuchukua uraia wa Ufaransa.