TaSUba yalia wasanii kutojiendeleza kielimu

Muktasari:

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Dk Herbert Makoye, anasema tatizo la wasanii kutopenda kujiendeleza kielimu halipo tu katika fani ya muziki bali kwa fani zote

Wasanii wengi duniani wamekuwa wakitumia vipaji pekee katika shughuli zao za kila siku bila kujiendeleza kielimu jambo ambalo limechangia kufifisha ndoto za wengi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Dk Herbert Makoye, anasema tatizo la wasanii kutopenda kujiendeleza kielimu halipo tu katika fani ya muziki bali kwa fani zote na ndio maana kuna madereva ambao kila leo wanakamatwa kutokana na kutopita katika mafunzo.

Pia wafyatua matofali nao sio wote wanaenda kujiendeleza katika vyuo vya ufundi(VETA) au machinga ni wachache sana wanaoamua kwenda kujiendeleza kimasomo katika masuala ya biashara.

Kikubwa ni kuendelea kuhamasishana kuhusu umuhimu wa elimu kwani mbali na kukusaidia katika kufanya kazi zao kiufanisi, inachangia kuwaongeza uelewa.

“Mfano kuna malalamiko mengi ya wasanii kuibiwa lakini ukija kuangalia awali alisaini mwenyewe mkataba, hivyo angekuwa amepita shule na kupata elimu ya haki miliki hayo yasingewakuta wengi,” alisema Dk Makoye.

“Shule hizi jamani zinakupa upeo na uelewa fulani wasanii wangepaswa kuja kukaa hata mwezi mmoja kwani hufungui sanaa yako tubali na ya ulimwengu kwani shule inakuchagiza hata kwenda kutafuta maarifa.”

Usikose kusoma mahojiano kamili kuhusu Taasisi hiyo katika Gazeti la Jumamosi, Desemba 15.