TFF yatoa sababu za kukacha kikao cha Mwakyembe

Thursday July 11 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa sababu za kushindwa kuhudhuria kikao cha Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ni kubanwa na majukumu mazito.

Kikao kilichoitishwa na Mwakyembe kilipangwa kufanyika Julai 10 mwaka huu, lakini wawakilishi wa TFF walishindwa kufika endeo la tukio kwa madai kuwa walibanwa na majukumu ya Shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alikiri kupokea taarifa za mwaliko wa mkutano huo kilichotakiwa kufanyika Julai 8, ambapo baadaye kilibadilishwa na kuwa Julai 9,vikao vyote hivyo viwili tulithibitisha ushiriki wao.

"Kabla ya kupata taarifa nyingine kutoka kwa wasaidizi wa Waziri ya kuwa kikao hicho kilisogezwa mbele tena hadi Julai 10 mwaka huu, tulijibu kupitia wasaidizi wake kuwa viongoziwa TFF wamebanwa na ratiba nyingine muhimu na nzito ambazo tayari zipo kwenye makubaliano na kuomba kupangiwa muda mwingine wa kikao."

"Tulitoa taarifa kwa wasaidizi wa Waziri kuwa mimi nitakuwa na  ratiba ya mapokezi na kazi kwa wakaguzikutoka FIFA kwa ajili ya ukaguzi wa fedha za FIFA kwa mwaka2018, ratiba ambayo tayari ilikwishapangwa kwa pamoja tangu Januari Mosi mwaka huu," ilisema taarifa ya TFF.

Taarifa hiyo iliongeza waliwajulisha kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia yupo nje ya nchi na Kaimu Makamu wa Rais Athuman Nyamlani atakuwa na kikao cha makubaliano na uongozi wa Fountain Gate Academy kuhusiana na timu zetu za taifa za Vijana.

Advertisement

Ilisema kikao hicho cha makubaliano na Fountain Gate Academy, kilihairishwa kutokana na tarehe za awali kugongana na tarehe ambazo Waziri alipanga kufanya vikao na TFF na hivyo haikuwezekana tena kuhairisha tena kutokuwa na mmiliki wa Fountain Gate Academy kuwa na safari za kikazi walishindwa kubadilisha tarehe tena.

Advertisement