TFF yasogeza siku ya mkutano mkuu

Thursday December 6 2018

 

By Mwandishi Wetu

 Dar es Salaam.  Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) iliyokutana Novemba 29,2018 imesogeza siku za Mkutano Mkuu uliokuwa ufanyike Desemba 30, 2018 mkoani Arusha na sasa utafanyika Februari 2,2019 jijini humo.

Sababu ya kusogezwa kwa mkutano huo ni kwendana sawa na kalenda ya uchaguzi mdogo uliotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Lindi na Mtwara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Simiyu na Shinyanga.

Zoezi la kuchukuwa na kurudisha fomu limeanza Desemba 4, 2018 na mwisho itakuwa Desemba 9, 2018.

Wenye sifa na uhitaji wa kugombea nafasi hizo fomu zikipatikana Makao Makuu ya TFF na kwenye tovuti ya TFF.

Advertisement