Sukari ya warembo

Muktasari:

  • Nyimbo nyingi zinazotungwa na mwanamuziki Diamond Platnumz zinapata mashabiki wengi kutokana na kuwa na uhalisia wa maisha ya mwanamuziki huyo.

DIAMOND bana, unaambiwa wimbo wake ukitoka, angalia hizo mbio za mashabiki kwenye Mainsta na Mayoutube, anakomba vijiji tu, hana mchezo.

Anavyoimba nyimbo zinazofanana na historia ya maisha yake kila siku, basi nyimbo hizo zimekuwa zikipokewa mashabiki kwa sababu zimeelezea kwa undani kabisa maisha yake ya mapenzi na maisha yake ya baadaeye.

Nyimbo zake kama; “Sikomi” na “Niache”, kuwataja wanawake wake wote ambao aliwahi kuwa nao katika mahusiano na vitendo vya kikatili walivyomfanyia katika mapenzi.

Upande mwingine, ana mambo makubwa. Hebu mfuatilie na hawa ni baadhi ya wanawake aliowataja Diamond katika baadhi ya nyimbo zake hizo:

WEMA SEPETU.

Aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, baadaye alikuja na kujiingiza katika tasnia ya bongo movies. Ni moja kati ya wasanii wa kike maarufu na wanaopendwa na kuongoza katika mitandao kuwa na mashabiki wengi sana.

Inadaiwa kuwa alikuwa na uhusiano na watu kadhaa maarufu na kila siku amekuwa ni mwanadada mwenye drama nyingi katika mapenzi.

Alishatoka na Mr. Blue, Idris Sultan, na Steven Kanumba.

Ukiachana na urembo lakini pia Wema anajihusisha na ujasiriamali wa vipodozi.

Amekuwa ni moja ya wanadada wanaojisifu kuwa na application inayoelezea maisha yake inayopatikana Playstore.

VJ PENNY

Kwa sasa ni mtangazaji wa kipindi cha harusi katika television moja nchini, jina lake lilipata umaarufu alipokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond.

Huyu ndie Diamond aliemlilia baada ya kupata mimba na kuitoa ilhali Diamond alikuwa akitamanai mtoto.

Hata hivyo, Diamond alisahau na kuendelea na maisha yake mengine kama kawaida, na baadaye alijikuta akiingia katika mahusiano mengine ya siri kabla ya kuja kuibuka tena.

HAMISA MOBETO

Baada ya kuendelea na watu wa kawaida wasiokuwa na majina, Diamond alikuja kuibuka kwa mwanadada mrembo huyu ambaye alikuwa akitumika kama modo katika matamasha mbalimbali.

Mobeto ni mwanamitindo ambaye kwa sasa amaeona fursa nyingine kupitia uigizaji na uimbaji, alikuwa na uhusiano na Diamond kwa muda mrefu lakini malavidavi yao yalikuwa ni siri kubwa, alikuja akapata mimba na Diamond aliikataa katika mitandao na vyombo vya habari.

Baada ya kutoa ushaidi wa mahusiano yao Diamond alikubali majukumu ya mtoto wa mrembo huyo. Ameingia katika vichwa vya habari kutokana na uhusiano wake na Diamond kwenda mrama hadi kufikia hatua ya kupelekana polisi. Amezaa na Diamond mtoto mmoja.

ZARINA HASSAN

Ni mama wa watoto watano lakini wawili amezaa na Diamond, ni mwanamke inasemekana kuwa amesaidia kwa kiasi kikubwa sana mafanikio ya msanii huyo ni mwanamama kutoka Uganda, mwenye utajiri mkubwa alioachiwa na baba mzazi wa watoto wake watatu wa kwanza.

Alipitia misukosuko mingi ya kiuhusiano na msanii Diamond lakini bado alijitahidi kuvumilia ili maisha yaendelee kutokana na mapenzi yake kwa kijana huyo wa Tandale.

Hata hivyo, alikuja kuchanganywa zaidi na Diamond baada ya kupata taarifa kwamba msanii huyo ametoka kimapenzi na Hamisa Mobeto huku kali zaidi ni baada ya Diamond kukubali mtoto wa Mobeto ndio ikawa kama tiketi ya Zari kuondoka.

Hivi, sasa kila mmoja na lwake hakuna tena mahusiano huku Diamond akitajwa katika mahusiano mbalimbali na wadada warembo.

Zari yuko Afrika Kusini akiendelea na maisha yake na wanwe hao.