Straika Simba aing'arisha Kagera Sugar

Thursday September 13 2018

By Saddam Sadick

Mwanza. Klabu ya Kagera Sugar imeitumia salamu Biashara United baada ya kuibamiza Pamba ya Mwanza mabao 4-3, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana Jumatano uwanja wa Nyamagana jijini hapa.

Mchezo huo ambao Pamba iliutumia mchezo huo kujiandaa na Ligi Daraja la kwanza (FDL), inayotarajia kuanza Septemba 29, wakati Kagera wao walijiweka sawa kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara utakaopigwa Jumamosi hii mjini Musoma mkoani Mara.

Straika wao ambaye pia aling'ara akiwa na Simba, Christopher Edward 'Edo' alipachika mawili dakika ya tatu na 37, Juma Shemvuni dakika ya 33, na Omary Dasashenko ya 44.

Mabao hayo, yalitosha kuwalaza wapinzani wao

 Pamba ambao mabao yao yalifungwa na  Geofrey Julius dakika ya 40, Kelvin John ya 58 na Frank Kilewa ya 67.

 

 

Advertisement