Straika Simba aibeba Coastal Union

Muktasari:

Ushindi huo unaifanya Coastal kufikisha pointi 4, baada ya kucheza mechi mbili kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Haji Ugando ameifungia timu yake Coastal Union bao pekee katika ushindi 1-0 dhidi ya Biashara United kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ugando alifunga bao hilo pekee katika dakika 20, baada ya kuwaahada mabeki wa Biashara United na kupiga shuti kwa mguu wa kushoto lililotinga nyavuni.

Katika mechi hii kulitokea matukio mawili ya utata la kwanza likiwa ni penalti waliyopata Coastal Union licha mpigaji wao kukosa, lakini Biashara nao walipata faulo dakika 45 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika mpira huo ulitinga nyavuni, lakini mwamuzi alikataa kwa kusema kuwa mchezaji wa mwisho aliogusa mpira huo alikuwa amezidi.

Ushindi huo unaifanya Coastal kufikisha pointi 4, baada ya kucheza mechi mbili kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Biashara wao baada ya kufungwa watabaki na pointi tatu ambazo walizipata baada ya kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua Singida.