Steve Nyerere, Irene Uwoya watinga Basata

Muktasari:

Katika kuitikia with wa Basata,wasanii Irene Uwoya na Steve Nyerere wamefika katika ofisi za Baraza hilo ambapo wanatarajiwa kuhojiwa kutokana na kitendo cha Uwoya kuwarushia fedha waandishi.

Dar es Salaam. Hatimaye wasanii wa filamu Irene Uwoya na Steve Nyerere wametinga katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa.

Wasanii hao wanafika katika ofisi hizo ikiwa ni kuitikia wito wa Baraza hilo walioupewa jana kutokana na kitendo cha Uwoya juzi  kuwarushia hela waandishi wa Habari wakiwa katika mkutano kati yao na wasanii wa Bongo Fleva.

Irene na Steve walitinga katika viwanja hivyo vya Basata saa 4:30 na gari aina ya prado nyeusi.

Kabla ya kushuka walikaa zaidi ya robo saa ndani ya gari huku waandishi waliofika hapo wakiwa wametegesha kamera zao kusubiri kuwachukua picha.

Hata hivyo ilipofika saa 4:45 wasanii hao walishuka kwenye gari hilo na kuelekea ndani ya ofisi ya Katibu Mtendaji wa Basata.