Stars yawasili katika joto la Cape Verde

Muktasari:

 Stars wamefikia katika hoteli ya Vipprai iliyopo kando kando mwa bahari ya Pacific na walipokelewa vema na wenyewe wao huku mashabiki wa Cape Verde wakionekana kutokuwa na chuki na msafara wa Stars kama ilivyozoeleka katika soka la Afrika.

Cape Verde.TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania jana iliwasili katika Jiji la Praia nchini Cape Verde kwa ajili ya kujiandaa na pambano la kufuzu michuano ya Afcon mwakani dhidi ya Cape Verde keshokutwa Ijumaa.

Stars imewasili leo Jumatano katika uwanja wa Ndege wa Nelson Mandela saa tano kamili kwa muda wa Cape Verde sawa na saa nane mchana kwa saa za Tanzania huku na kupokelewa na joto kali la jiji la Praia huku wachezaji wa timu hiyo wakiahidi ushindi.

Kabla ya Stars kuwasili jana tayari juzi staa wa kimataifa wa Tanzania anayecheza Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta na staa mwingine, Simon Msuva anayecheza klabu ya Jadida ya Morocco walikuwa wamewasili na kuungana na wenzao waliofikia hoteli ya Praia.

Kocha, Emmanuel Amunike alidai kwamba lengo lao kubwa ni kushinda katika pambano la kesho kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya miaka 38 bila ya kufanya hivyo.

“Natazamia kwamba tunaweza kushinda mechi ya kesho kama wachezaji watafuata maelekezo yangu lakini siku zote mechi za ugenini huwa ni ngumu kwa mgeni. Tutapambana kama tulivyofanya kwa Uganda.” Alisema Amunike.

Naye mlinzi wa kimataifa wa Stars, Abdu Banda anayekipiga katika klabu ya Boroka ya Afrika Kusini alidai kwamba lengo lao kubwa ni kufanya vema katika mechi ya kesho.

“Tunamshukuru Mungu tumefika salama na tumekuja kupambana kwa ajili ya mechi ya keshokutwa (Kesho). Tunamuona Mwenyezi Mungu atuombee tu.” Alisema Banda.