Stars, Kenya zatangulia nusu fainali

Muktasari:

  • Stars ina pointi tatu ambazo ilizipata katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zanzibar Heroes.

TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' inmetinga nusu fainali ya michuano ya Chalenji baada ya kutoka suluhu dhidi ya Sudan mechi iliyomalizika muda mfupi Uwanja wa KCCA jijini hapa.
Stars imeingia hatua hiyo pamoja na Kenya kutoka kundi lao B ambayo imefunga Zanzibar bao 1-0 mchezo ulioanza kuchezwa leo Jumamosi saa 7.30 mchana kwenye uwanja huo.
Kilimanjaro Stars ilikuwa inahitaji angalau matokeo ya sare tu ili kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Kilimanjaro Stars na Sudan zilikwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu ambapo hakuna mmoja aliyeona lango la mwenzake ingawa Stars walionekana kutawala mchezo na kutengeneza idadi kubwa ya nafasi ambazo hata hivyo safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kuzitumia.
Mapema tu dakika ya 21, Stars ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Miraji Athuman kuumia na nafasi yake ilichukuliwa na na Cleoface Mkandala.
Katika kipindi hicho mchezaji Magid Abdellatef wa Sudan alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu, Mzamiru Yassin.
Timu hizo mbili sasa zitawasubiri washindi kutoka Kundi A ambao mechi zao zitachezwa