Stand United yatibua rekodi ya Yanga, ikiifunga mabao 1-0

Muktasari:

Awali, timu zilikwenda mapumziko huku pengo la mshambuliaji Heritier makambo ambaye leo alianza benchi likionekana.

Shinyanga. Timu ya Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza Ligi Kuu mbele ya wenyeji wao Stand United baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Katika mchezo huo bao la ushindi la Stand United kwenye mchezo huo lilifungwa na Strains Jacob Masawe dakika ya 87.

Awali, timu zilikwenda mapumziko huku pengo la mshambuliaji Heritier makambo ambaye leo alianza benchi likionekana.
Makambo ambaye hakuwepo takribani wiki mbili sasa alianzia benchi katika mchezo huu wa leo dhidi Stand United.
 Krosi zote ambazo zinapigwa na Ibrahim Ajib zilikuwa zikikosa mmaliziaji tofauti na anapokuwepo Makambo ambaye alikosekana kipindi cha kwana.
Hata hivyo mashabiki wa Yanga walianza kushangilia baada ya Makambo kuanza kupasha lakini hakuweza kuingia kwa wakati huo ambapo dakika za kipindi cha kwanza zilikuwa zinaelekea ukingoni.
 Safu ya ushambuliaji ya Yanga leo iliongozwa na Amis Tambwe, Haruna Moshi, Mrisho Ngassa.