Soni FC bingwa Junior Cup Tanga

Muktasari:

Waziri Junior amekuwa na kawaida ya kuanzisha kombe nyumbani kwao Tanga kwa ajiili ya kuendeleza vipaji vya mkoani humo.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Waziri Junior amekumbuka vijana wenzake wa nyumbani kwao Lushoto, Tanga baada ya kuweka kombe ambalo litakutanisha timu za mtaani kwao.

Baada ya kuchezwa mechi mbalimbali, leo jioni imechezwa fainali ya mashindano hayo yanayoitwa 'Junior Cup' huku timu ya Soni Fc ikiichapa Yoghoi Fc  kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya awali kutoka sare ya 1-1.

Bingwa wa kombe hilo (Soni) amepata zawadi ya mbuzi wawili na mpira mmoja, huku mshindi wa pili Yoghoi Fc akipata Mbuzi na mpira mmoja kama zawadi ya kufika hatua hiyo.

Kwa upande wa mshindi wa tatu alipata mpira mmoja huku mfungaji bora wa mashindano akipata pesa taslimu shilingi elfu thelathini kama zawadi (30000).

Junior amekuwa na kawaida ya kuanzisha kombe kwao Lushoto mara kwa mara kwa vijana wenzake ili kuendeleza soksa na kuinua vijana wenzake ambao bado wanacheza soka la mtaani.