Song afichua fedha ilivyomng'oa Arsenal

Tuesday May 19 2020

 

London, England. Kiungo wa zamani wa Arsenal, Alex Song ameweka wazi kuwa hakufikiria mara mbili kufanya  maamuzi ya kuondoka  Arsenal na kwenda Barcelona baada ya kutangaziwa mshahara mnono.
Raia huyo wa Cameroon alitimka Arsenal na kwenda Barcelona kwa ada ya uhamisho wa Pauni  15 milion msimu wa joto wa 2012.
Hatua ya kwenda Hispania kulimfanya kiungo huyo kati kupata ongezeko la mshahara kutoka Pauni 55,000 alizokuwa akilipwa kwa wiki ndani ya Arsenal hadi Pauni 70,000.
Song (32) ameeleza kuwa uamuzi aliochukua miaka nane iliyopita haukuwa mgumu kutokana na nguvu ya fedha.
'Nilikutana na mkurugenzi wa michezo wa Barcelona na akaniambia sitopata nafasi ya kucheza michezo mingi,
Nilijua kuwa sasa nitakuwa milionea, sikuyapa nafasi aliyokuwa akiyasema Mkurugenzi. Wakati Barcelona ilinipa mkataba, na nikaona ni pesa nyingi , sikufikiria mara mbili.
"Ninasema kila wakati, kijana wa miaka 20 ambaye anaendesha  Ferrari  maisha yake ni  duni kwa sababu haujafanya chochote bado. Lakini mtu wa miaka 50 ambaye anaendesha gari  la maana  'Bentley', ni mtu wa kumheshimu." alisema
Song pia ameelezea jinsi alivyopigwa  na butwaa pindi ambapo alipoliona gari la Thierry Henry alipofika mazoezi.
"Nilipofika Arsenal, nilienda mazoezini  kisha nikaona mfalme akifika (Thierry Henry) akiwa na gari lakini adhimu, gari lilikuwa la thamani mno.Nilijiambia kuwa ninahitaji gari ile ile kwa gharama yoyote.
Niliporudi siku nyingine mazoezini akaniuliza gari yako iko wapi nilimweleza kuwa haiendani na hadhi yangu. Niliachana nayo kwa sababu niliona inanimalizia mafuta bure." alisema Song.

Advertisement