Solskjaer sasa apewa Arsenal Kombe la FA

Wednesday January 9 2019

 

London, England. Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United, atakutana uso kwa uso na Arsenal katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la FA.

Ratiba iliyotolewa juzi usiku inaonyesha Man United itavaana na Arsenal, mchezo ambao utakuwa mtihani mwingine mgumu kwa kocha huyo wa muda.

Solskjaer alikuwemo katika kikosi cha Man United kilichoshinda mechi mbili za nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal mwaka 1999 na 2004.

Mechi hiyo ya nusu fainali ya Kombe la FA itachezwa kati ya Januari 25-28 na Arsenal itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Emirates.

Advertisement