Solskjaer asifu kikosi Man United, Barcelona ikitinga nusu fainali Ulaya

Muktasari:

Mabao ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Lionel Messi dakika ya 16 na 20 kipindi cha kwanza. Msumari wa tatu ulishindiliwa na Philippe Coutihno.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar amesema kikosi chake kimeonyesha kiwango kizuri kufika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa, huku ikiondolewa hatua hiyo baada ya kufungwa na Barcelona mabao 3-0 jana Jumanne usiku.

Barcelona imetinga nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-0. Awali robo fainali ya kwanza iliyochezwa wiki iliyopita Barcelona ilichomoza na ushindi wa bao 1-0.

Mabao ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Lionel Messi dakika ya 16 na 20 kipindi cha kwanza. Msumari wa tatu ulishindiliwa na Philippe Coutihno.

Kocha huyo wa Manchester United aliyethibitishwa klabuni hapo hivi karibuni, alikisifu kikosi chake kwa hatua ya robo fainali waliyofika.

Amesema changamoto iliyopo mbele yake ni kuhakikisha  timu yake inamaliza kwenye nafasi nne za juu Ligi Kuu England ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki tena mashindano hayo.