Solskjaer ana siku mbaya zaidi Man Utd

Manchester, England. Kocha Ole Gunnar Solskjaer ameeleza kuwa kipigo cha Manchester United cha mabao 6-1 dhidi ya Tottenham Hotspur kimefanya kuwa na siku mbaya zaidi katika maisha yake ya soka kama kocha. Penalti ya Bruno Fernandes iliipa Man United uongozi dakika ya pili ya mchezo, lakini mambo yalibadilika na kushuhudia wenyeji wakimaliza mchezo kwa kuchapwa mabao sita, huku vijana wa Jose Mourinho wakizima tambo za Old Trafford.

Kipigo hicho cha Jumapili kiliongeza presha kutokana na kutokuwa na usajili wa kueleweka, wiakati mabosi wa Man United ikishindwa kumsajili Jadon Sancho, ambaye alikuwa akitakiwa na Solskjaer.

Kocha wa Man United alionyesha masikitiko yake katika kipigo hicho kikubwa nyumbani katika historia ya Ligi Kuu, kikiwa ni kama kile dhidi ya Man City cha 6-1 cha 2011.

“Ni matokeo ya kuudhi,” alikiri Solskjaer. “Hii ni ligi yangu ya pili kufundisha hivyo ni ngumu kuelezea. Najisikia vibaya, siku mbaya zaidi kuiwa kocha wa Manchester United na mchezaji.

“Niliwahi kuwa sehemu ya kipigo kikubwa kabla ya hii na huwa tunarudi mchezoni, niwaache vijana waende katika timu zao za taifa, wakatulize vichwa na kurudi wakiwa wapya.

“Hatuko karibu na afadhali. Unapofungwa kama hivi unatakiwa kujitazama katika kioo.”

Kipigo hicho kimeongeza presha katika bodi ya klabu kwa kutaka sura mpya kikosini kabla ya usajili kufungwa jana usiku.

Man United ilikuwa karibu kumalizana na Edinson Cavani kama mchezaji huru.