Solskjaer akabidhiwa mzigo, kuanza na Sancho, Grealish

Saturday February 15 2020

Solskjaer akabidhiwa mzigo, kuanza na Sancho, Grealish, Ole Gunnar Solskjaer ,winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho,

 

MANCHESTER United itamkabidhi Ole Gunnar Solskjaer Pauni 274 milioni kuimarisha kikosi chake pindi dirisha la usajili la kiangazi litakapofunguliwa, huku Pauni 100 milioni kati ya hizo zikitarajiwa kutumika kwa winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho.

Licha ya kutumia zaidi ya Pauni 220 milioni tangu akabidhiwe timu, Solskjaer ameshindwa kukitengeneza kikosi cha ushindi, lakini bado uongozi wa Man United una imani naye ndiyo maana umemtengea Pauni 274 milioni zaidi ili aimarishe timu wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Inaelezwa mbali na Sancho, Pauni 160 milioni nyingine zitatumika kwa ajili ya kuwanasa mastaa wawili wa England, Jack Grealish kutoka Aston Villa na James Maddison wa Leicester City.

Man United pia inatafuta straika wa kutoa changamoto kwa Marcus Rashford na Anthony Martial na ndiyo maana timu hiyo inatajwa kuandaa ofa ya kumng’oa Moussa Dembele kutoka Olympique Lyonnais.

Advertisement