Solskjaer Krismasi inaweza isifike

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameibukia kwenye orodha ya makocha wa Ligi Kuu England wanaoweza kufutwa kazi na timu zao kabla ya Krismasi baada ya kupigo kizito kutoka kwa Tottenham.

Kocha huyo yupo kwenye presha kubwa kwa sasa baada ya mechi tatu tu alizochez kwenye ligi, akipoteza mechi mbili na kushinda moja.

Jambo linalotisha ni kwamba kwenye mechi hizo tatu, kikosi hicho cha Old Trafford kimeruhusu wavu wao kuguswa mara 11, jambo linalowafanya wacheza kamari kudhani Kocha Solskjaer yupo kwenye hatari ya kupoteza ajira.

Kipigo hicho cha mabao 6-1 kutoka kwa Spurs juzi Jumapili, kimewafanya Man United kushika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi. Kwa mabao 11 iliyoruhusu, inakuwa timu ya pili kuruhusu wavu wake kuguswa mara nyingi kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Wacheza kamari wanaamini kwamba kwenye nafasi 13 za kufukuzwa, Solskjaer ana nafasi nane za kufunguliwa mlango wa kutokea kabla ya Krismasi. Kocha huyo wa zamani wa Molde ana nafasi moja kati ya mbili ya kufutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.

Kwa maana hiyo, Solskjaer ni kocha namba mbili kwenye hatari ya kufutwa kazi baada ya Scott Parker wa Fulham, ambaye ana nafasi nane kati ya 11.

Baada ya kipigo cha Spurs, Solskjaer alisema: “Ile 2-1 tulikuwa bado mchezoni, baada ya kadi nyekundu kila kitu kiliharibika.

“Huwezi kushinda mechi kwa kufanya makosa kama haya na kucheza kwa kiwango kama kile. Ni udhalilishaji mkubwa, ni kosa langu. Sio kocha la Manchester United.

“Sio jambo la kusajili wachezaji ni jambo la nani yupo. Hii ilikuwa mbaya sana, siwezi kusema zaidi ya hilo.

“Unapokuwa nyuma kwa 2-1 unakuwa na nfasi, nyuma kwa 3-1 inakuwa ngumu. nyuma kwa 4-1 inakuwa mbaya zaidi.Tunahitaji kurekebisha kila kitu.”

Makocha wengine wenye nafasi kubwa ya kufutwa kazi ni Sean Dyche, David Moyes na Frank Lampard.