Solskjaer: Lukaku wa kazi gani?

Friday August 9 2019

 

MANCHESTER, ENGLAND.Kocha Ole Gunnar Solskjaer kaibuka na kusema kuwa anaamini Manchester United itakuwa poa  zaidi bila ya Romelu Lukaku, ambaye ametimkia Inter Milan kwa ada ya Pauni 74 milioni.
Kocha huyo amesema kuwa kuondoka kwa wachezaji hao kunatoa mwanya kwa nyota Mason Greenwood na Alexis Sanchez kuonyesha kiwango chao.
 “Nadhani ulikuwa wakati mwafaka kwa yeye (Lukaku) kuondoka. Kizuri ni kwamba tumepata dili zuri ambalo limenufaisha kila upande.
Kila mmoja ana furaha. Kuna wakati Lukaku aliumia, hakuwa na wakati wa kucheza. Nadhani atakwenda kuwa na mwanzo mpya pale Inter Milan.
“Kaondoka lakini tunaendelea, nadhani tutapata mabao mengi kutoka kwa Anthony Martial, Marcus Rashford, Dan James au Jesse Lingard. Tuna washambuliaji wazuri tu. 
“Kuelekea mwisho wa msimu uliopita hatukuwa tukifunga mabao ya kutosha lakini tunaamini tutafanya vyema katika msimu huu.”  

Advertisement