Solskajer abariki Sanchez kusepa Manchester United

Muktasari:

Sanchez anahusishwa kuwa katika maongezi na Inter Milan kwa mkopo pia kukiwa na kipengele cha kumuongezea mshahara.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameweka wazi kama mchezaji wake Alex Sanchez anataka kuondoka anatakiwa kufanya katika kipindi hiki cha usajili.

Sanchez anahusishwa kuwa katika maongezi na Inter Milan kwa mkopo, pia kukiwa na kipengele cha kumuongezea mshahara.

Akizungumza baada ya sare dhidi ya Wolves, Solskajer alisema bado kuna wiki zilizobaki za usajili ambazo mchezaji huyo anaweza kuzitumia.

"Kuna timu ambazo zimeonyesha kumuhitaji Sanchez, kama anataka kuondoka ndio muda huu lakini tusubili kuona nini kinatokea," alisema.

Solskajer aliongeza licha ya kwamba hivi sasa Sanchez ni mchezaji wao, anasubili kuona nini ambacho kitatokea katik siku za hivi karibuni.

Sanchez anatarajiwa kufanya vipimo vya afya leo Jumanne katika klabu ya Inter na kusajiliwa kwa mkopo huku kukiwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja.