Sol Campbell amchana beki Van Dijk

LIVERPOOL, ENGLAND. BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell amesema beki wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk bado ana kiwango kikubwa lakini kinachomkwamisha ni kuridhika kwake kwa sababu hakuna mchezaji mwingine ambaye anaonekana kushindana naye katika eneo lake.

Mchezaji huyo ambaye ameonekana kuwa kwenye kiwango kibovu katika siku za hivi karibuni na kusababisha timu yake kuwa katika hali mbaya, ni miongoni mwa mabeki ambao walionyesha kiwango kikubwa katika misimu kadhaa iliyopita.

“Ni mchezaji mzuri na anayetambua vyema majukumu yake awapo uwanjani lakini shida ni kuwa hajapata mtu wa kugombania naye namba hii inamfanya aridhike sana,” alisema.

“Kama huna safu nzuri ya ushambuliaji, uwe na safu ya bora ya ulinzi,” alisema.