Sofapaka waitesa Gor Mahia KPL

Muktasari:

Bao hilo la penalti, lililofungwa na Mganda Umaru Kasumba, imeipeleka kileleni mwa Jedwali baada ya kufikisha pointi 48, pointi mbili mbele ya Mabingwa watetezi Gor Mahia.

RAUNDI hii wamekuja vibaya sana buda. Mabingwa wa KPL, mwaka 2009, klabu ya Sofapaka wamekuja kuchukua hii kitu na hawataki mchezo na mtu.

Baada ya kucheza mechi yao ya 25, kikosi cha Sofapaka, kinachonolewa na kimeendelea kung’ang’ania uongozi wa jedwali la msimu huu wa KPL, ambapo wakiwa katika uwanja wa ugenini, huko Green Stadium Awendo, waliichapa Sony Sugar 1-0.

Bao hilo la penalti, lililofungwa na Mganda Umaru Kasumba, imeipeleka kileleni mwa Jedwali baada ya kufikisha pointi 48, pointi mbili mbele ya Mabingwa watetezi Gor Mahia.

Kwa upande wao, kipigo hicho ambacho ni cha kwanza, katika michezo mitatu ya hivi karibuni, kiliwafanya wakata miwa hao wa Awendo, kukaa

katika nafasi ya saba, wakiwa na pointi 35.

Huko Kisumu, Vijana wa Hassan Oktay, walijikuta wakivutwa nguo na wanajeshi wa KDF, klabu ya Ulinzi Stars, matokeo ambayo yaliwafanya washuke hadi nafasi ya pili, wakiwa na pointi 46, lakini wakiwa na michezo minne mkononi.

Dennis Oliech ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwapatia Kogalo bao, katika dakika ya 46 ya kipindi cha pili, lakini bao hilo lilidumu kwa dakika 10 pekee, kwani Ulinzi walisawazisha kwa Penalti, lilipigwa na straika wao hatari, aliyekuja na ubaya msimu huu, Enosh Ochieng.

Katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos, Posta Rangers waliwatandika Zoo Kericho 2-0, Vihiga United wakilazimishwa sare ya 2-2 na Mathare

United, katika mchezo mwingine wa Jumapili, uliopigwa huko Mjini Kakamega katika uga wa Bukhungu.

Kwa matokeo ya Jumapili, mbio za ubingwa zimeendelea kuwa ngumu, huku Sofapaka, Gor Mahia na Bandari zikionekana kupelekana mbio kwelikweli.

Sofapaka wanaongoza na pointi 48, Gor Mahia ambao wana mechi nne mkononi, wakiwa wa pili na pointi 46.

Bandari, ambayo wikendi hii haikucheza, inashika nafasi ya tatu na pointi 45, Mathare United, baada ya kulazimishwa sare na Vihiga United, inasalia katika nafasi ya nne, ikiwa imeongeza pointi moja,

ambayo inawafanya wafikishe pointi 39.