Singida yajisalimisha TFF

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga alisema tayari wameshatuma maombi yao TFF.

UONGOZI wa Singida United umetua kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuomba mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Coastal Union uchezwe Uwanja wa Azam Complex badala ya Namfua kwa kuwa ratiba imebana.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga alisema tayari wameshatuma maombi yao TFF.

Aliongeza, jana Jumatano, Singida ilitakiwa kucheza Ndanda mjini Mtwara na mara baada ya mchezo huo leo Alhamisi itakuwa njiani kurudi Singida ambayo ni safari ya siku mbili, hivyo ingefika Ijumaa usiku wakati Jumamosi inatakiwa kucheza na Coastal.