Sinema ya Neymar, Najila kama Telenovela

Muktasari:

Najila aliwasilisha kesi hiyo akidai kulipwa fidia ya zaidi ya Pauni 200,000 (Sh20 milioni) kwa madai hayo ya kubakwa.

MASINEMA kati ya nyota wa PSG Mbrazil Neymar na mwanamitindo aliyedai alimbaka, Najila Trindade bado zinaendelea utadhani ni kipindi cha telenovela vile.

Sasa baada ya kesi kumgeukia Najila kwa jaji aliyekuwa akisikiza kesi hiyo kusema mwanamitindo huyo atashtakiwa kwa kutoa taarifa za uwongo kuhusu madai yake ya kubakwa na nyota huyo, dada huyo naye kaanza kupambana.

Wakili wake Najila. Cosme Araujo sasa kasema nao wataelekea mahakamani kupinga uamuzi huo wa kumshtaki mwanamitindo huyo.

Jaji huyo kasisitiza ni lazima sheria imchukulie hatua Najila kwa kitendo alichokifanya ambacho ni dhahiri madai yake yalikuwa ya udanganyifu yaliyolenga kutekeleza utapeli.

Najila aliwasilisha kesi hiyo akidai kulipwa fidia ya zaidi ya Pauni 200,000 (Sh20 milioni) kwa madai hayo ya kubakwa.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi wa kina wa miezi kadhaa, waendesha mashtaka waligundua Najila hakubakwa na kuwa alikubali kuingia kwenye mahusiano na nyota huyo pasi na kushurutishwa na yeyote.

Baada ya uchuguzi huo kukamilika, kesi hiyo ilifutwa na faili kufungwa.