Sina tatizo na Ajibu-Sven

Tuesday June 2 2020

 

Siku moja baada ya kumrejesha kundini Ibrahim Ajibu, kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa hana tatizo lolote na mshambuliaji huyo.
Sven alimtimua Ajibu wiki iliyopita baada ya mshambuliaji huyo kuchelewa kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michezo iliyobakia ya Ligi Kuu.
Akizungumza na Mwanaspoti Online, Vandenbroeck alisema hatua alizozichukua dhidi ya Ajibu zililenga kumjenga na mchezaji huyo na haimaanishi vingine.
"Ajibu amerudi kambini tena akiwa katika hali nzuri na ushindani kama wachezaji
wengine ila tumemfanyisha mazoezi akiwa na mwenzake Kahata (Francis) kwani ndio siku ya kwanza wanafanya mazoezi ya pamoja uwanjani akiwa na wenzake.
Kwa maana hiyo ilikuwa lazima wafanye kwanza wenyewe ili kuwa kiwango sawa na wenzao walioanza tangu wiki iliyopita.
Kiujumla Ajibu yupo sawa wala hana shida au tatizo na anaendelea na majukumu
yake kama ilivyo wachezaji wengine wote," alisema Vandenbroeck.
Mbali na adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria mazoezi, Ajibu pia alipigwa faini ya Sh 200,000 kwa kosa lake hilo.

Advertisement