Simba yawaita mashabiki Taifa kuikabili Nyasa Big Bullet

Muktasari:

  • Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet

KLABU ya Simba imetaja viingilio vitakavyotumika katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa, ambapo kiingilio cha chini ni Sh 3,000 na cha juu Sh 1,0000.

Akizungumza Dar es Salaam Jana, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema Sh 3,000 kitatumika katika viti vya machungwa, kijani na bluu ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kujitokeza kuishangilia timu hiyo.

Pia, alisema Sh 7,000 ni kwa ajili ya VIP B na C huku Sh 10000 ikiwa ni VIP A na wakati huo huo, akihimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangilia timu yao ambayo inayojiandaa na ligi pamoja na mashindano ya kimataifa.

“Tunatambua mchango na thamani ya mashabiki wetu ndio maana tumeweka kiingilio kidogo kwa viti vingi ili washiriki kikamilifu katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa kumi nambili jioni katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam,”alisema.