Simba yaishusha Yanga kileleni ikiipasua Mtibwa Sugar mabao 3-0

Thursday May 16 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Alhamisi.

Mabao ya Simba yaliwekwa wavuni na John Bocco (32),  Clatous Chama (47) na Emmanuel Okwi (57).

Ushindi huo unawapeleka Simba kileleni baada ya kufikisha alama 85, huku Yanga wakivutwa hadi nafasi ya pili wakiwa na alama 83.

Mtibwa Sugar inasalia nafasi ya 5 ikiwa imejikusanyia alama 49

Kipindi cha kwanza kati ya Simba na Kagera Sugar kilimalizika kwa Simba kuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao la Simba lilifungwa dakika 32 na John Bocco ambaye alifikisha jumla ya mabao 15, msimu huu.

Kipindi cha kwanza Simba wakionekana kushambulia mara kwa mara lakini walishindwa kutumia nafasi nyingi.

Simba mbali ya kukosa nafasi nyingi kupitia kwa Maddie Kagere, Bocco na Emmanuel Okwi.

Mbali ya nafasi hizo nyingi Simba walionekana kupata kona nyingi ambazo nazo walishindwa kuzitumia.

Mtibwa Sugar wao walipata nafasi chache kuliko Simba ambazo hazikuwa hatari zaidi.

Muda mwingi Mtibwa walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza ambayo kipa wa Simba Aishi Manula alikuwa akiyadaka.

 

 

Advertisement