Simba yaanza moto upyaaa

Muktasari:

Ushindi wa 5-0 dhidi ya Mwadui FC, unakuwa ni ushindi wa kwanza mkubwa katika kikosi cha Simba msimu huu.

USHINDI wa 5-0 waliopata Simba dhidi ya Mwadui umerejesha furaha kwa mashabiki wa Simba baada ya kuwa na kiu ya ushindi kutokana na kukosa furaha katika michezo miwili waliyofungwa mfululizo.

Simba awali ilipoteza katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons (1-0) na Ruvu Shooting wakipoteza kwa bao moja katika kila mchezo.

Ushindi huo unawafanya Simba kukusanya pointi 16 na kutoka nafasi ya tano na kusogea mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi.

Katika kipindi cha kwanza Simba walishinda bao moja lakini katika kipindi cha pili baada ya mabadiliko waliweza kufunga mabao manne.

Mwadui kwenye kipindi cha kwanza walicheza kwa kujilinda zaidi na kuwafanya Simba wapate wakati mgumu lakini kitendo cha kufunguka

Kwenye kipindi cha pili Simba waliendelea kutengeneza nafasi lakini umakini ulikuwa mdogo.

Dakika 55 mshambuliaji wa Simba, John Bocco alikosa goli la wazi baada ya kupigiwa krosi na Mohamed Hussein 'Tshabalala' na kushindwa kuunganisha kwa mguu.

Safu ya ushambuliaji Simba ilionekana kuzidiwa na mabeki wa Mwadui waliokuwa wanasimamiwa na nahodha wao Joram Mgeveke japo hapakuwa na madhara langoni kwao.

Dakika 57 kiungo Rally Bwalya alipiga shuti kali akiwa nje ya boksi lakini kipa wa Mwadui FC, Musa Mbisa aliucheza mpira huo na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Mshambuliaji John Bocco wa Simba katika mchezo huu ni kama vile alikuwa hana bahati toka kipindi cha kwanza kwani licha ya kutengenezewa nafasi mara kwa mara.

Simba dakika 60 walifanya shambulizi lililoanzia kwa Shomari Kapombe aliyepiga pasi mpenyezo kwa Clatous Chama ambaye alituliza mpira na kupiga pasi ya chini ndani ya boksi lakini Bocco aliunganisha mpira na kupaa juu.

Dakika 60 Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Rally Bwalya na kuingia Hassan Dilunga kwenda kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.

Mabadiliko hayo yalijibu ndani ya dakika nne baada ya ya kiungo Clatous Chama kumpigia pasi Hassan Dilunga ambaye alikuwa ndani ya boksi eneo ambalo alikiwa na uwezo wa kupiga lakini alimpigia pasi John Bocco aliyepiga shuti na kwenda moja kwa moja wavuni.

Mwadui walifanya mabadiliko dakika 68 kwa kumtoa Jackson Shiga na kuingia Lillah Hussein, wakati huo huo Simba walifanya mabadiliko dakika 70 kwa kumtoa John Bocco na kuingia Ibrahimu Ajibu.

Baada ya kuona mipango haiendi, Mwadui walifanya mabadiliko 77 mengine kwa kumtoa Abas Kapombe na Charles Masenga huku nafasi zao zikichukuliwa na Wallace Kiango na Amri Msenda.

Simba ilipata bao la tatu kupitia kwa Ibrahimu Ajibu aliyefuatuka shuti kali baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Hassan Dilunga.

Dakika 89 Simba nusu wapate bao la nne baada ya Shomari Kapombe kupiga pasi ndani ya boksi iliyokutana na Hassan Dilunga ambaye na yeye alipiga pasi nyingine iliyoenda kukutana na Ibrahimu Ajibu lakini alipiga shuti lililokwenda juu.

Hata hivyo Dilunga alifuta makosa hayo kwa Ajibu ndani ya dakika moja tu (90) baada ya kuifungia Silba bao la nne akiingia ndani ya boksi na kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Wakati huo huo dakika 90 Simba ilimtoa Clatous Chama na kuingia Francis Kahata, lakini mabadiliko hayo hayakuwa na nguvu kwa upande wake.

Baada ya magoli hayo Mwadui walionekana kutokuwa na mbinu mbadala kwani walionekana kucheza bila kuwa na mipango.

Dalika 92 Simba ilipata bao la tano lililofungwa na Said Ndemla aliyefyatuka shuti kali na kwenda wavuni