Simba wapikwa kukaba

Muktasari:

  • Aussems alitaka wachezaji wake wapasiane kwa haraka na waliokuwa wanakaba kwa nguvu ili kupora mipira hiyo.

Wachezaji wa Simba baada ya kumaliza mazoezi ya viungo walihamia katika mazoezi mengine.

 Mazoezi waliyohamia ni yale ya kucheza kwa kukaba yaani wachezaji saba wanakuwa ndani na wengine nane wanakuwa pembeni wakipasiana ili wale wa kati wasiupate mpira.

Kocha wa Simba Patrick Aussems alionekana kuwa mkali kwa mchezaji ambaye anakosea kupiga pasi au kupoteza mpira.

Aussems alitaka wachezaji wake wapasiane kwa haraka na waliokuwa wanakaba kwa nguvu ili kupora mipira hiyo.

Pindi walipokuwa wanakosea alikuwa mkali na hata kutoa maneno kwa sauti ya juu kwa kuwafokea.