Simba wapiga tizi la kufa mtu

Muktasari:

Simba watafanya mazoezi ya mwisho kesho saa 3:00 asubihi na mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo nyota wote wataingia kambini katika Hoteli ya Sea Scape kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Big Bullets ya Malawi.

Kikosi cha Simba mbali ya kuwakosa nyota wao wengi waliokuwa katika timu zao za Taifa wanaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans.
Simba watafanya mazoezi ya mwisho kesho saa 3:00 asubihi na mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo nyota wote wataingia kambini katika Hoteli ya Sea Scape kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Big Bullets ya Malawi.
Big Bullets ni mabingwa mara 12 wa ligi ya Malawi lakini mabingwa hao watetezi wa Tanzania wameendelea kufanya mazoezi ya nguvu na yale ya kucheza soka muda mrefu.
Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema wanaendelea na mazoezi ili kila mchezaji aweze kuwepo katika kiwango bora na ufuti ule ule.
"Waliokuwa katika kambi ya timu ya Taifa wanafanya mazoezi na ndio maana waliobaki hapa nao wanafanya ili kulingana nao na watakapo kuwa pamoja kazi inakuwa ile ile kama hapo awali," alisema.
Simba wiki iliyopita walifanya mazoezi ya nguvu ndani ya Gym viwanja vya Gymkhana na walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya vijana ya Azam ambao waliwafunga bao 1-0 lililofungwa na Said Ndemla.